Header Ads

Header ADS

Serikali kuajili maafisa afya Wa Mazingira mwakani

Hayo yamesemwa na  waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu amesema serikali ya awamu ya sita ina lengo la kuajiri maafisa afya mazingira katika kila kata kama sera ya afya inavyoeleza.

Waziri Ummy amesema hadi sasa Tanzania ina kata 4263 huku kata zenye maafisa afya mazingira ni 1305 ambapo amesema ajira za mwakani serikali itahakikisha namba hiyo inaongezeka

Kauli hiyo ameitoa leo katika kilele cha maadhimisho ya miaka mitano ya kampeni ya Nyumba ni Choo, iliyofanyika Jijini Dar es salaam

“Nataka ajira za mwakani na niombe Mungu niendelee kuwa waziri wa afya na Rais aendelee kuniamini naenda kuhakikisha hili linafanikiwa”amesema waziri Ummy

Waziri huyo amesema kuwa tumekuwa tukiangalia sana madaktari, wauguzi, mganga lakini hatuangalii tuna maafisa afya mazingira wangapi

Amesema lengo kuu la serikali ni kuhakikisha kuwa kila kata inakuwa na angalau afisa afya mmoja ikiwa ni takwa la sera ya afya ya Tanzania

Katika hatua nyingine waziri Ummy amewataka watanzania kuwa na desturi ya kuthamini vyoo vyao na kuvifanya kuwa visafi 

“Watanzania wengi tunadharau choo, hatuthamini choo ila choo ni sehemu ya kutulia na ikiwezekana choo ni sehemu ya kuondoa stress” 

Katika kilele hicho cha maadhimisho ya nyumba ni choo Halmashauri ya Nombe imeongoza kwa kuwa na vyoo safi ikifuatiwa na halmashauri za Iringa na Moshi 

Aidha katika mikoa inayoongoza kwa kuwa na vyoo bora ni Kilimanjaro yenye asilimia 89, Iringa yenye asilimia 87.7 na Njombe yenye asilimia 86

Waziri Ummy Mwalimu amesema Kampeni ya nyumba ni choo imefanikiwa kwa asilimia 72.1 kutoka asilimia 

No comments

Powered by Blogger.