BRELA yawasisitiza wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kwa mazoea
Wafanyabiashara nchini wametakiwa kuacha kufanya biashara kwa mazoea na badala yake wafuate sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na kusajiri jina la biashara au kampuni ili kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya wafanyaiashara na wamiliki wa makampuni.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Leseni kutoka Wakala wa Usajili na Leseni BRELA Bi. Sweetness Madatu wakati wa maonyesho ya tano ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyofanyika Mkoani Morogoro .
Kwa upande wao wakazi wa Mkoa wa Morogoro waliotembelea banda la BRELA katika viwanja vya Jamhuri wameupongeza wakala huo, kwa elimu wanayoitoa kwa wananchi hao juu ya Umuhimu wa kusajili Bishara zao katika mamlaka hiyo.
Wakizungumza na Waandishi wa habari wakazi hao wamesema kuwa licha ya kusogezewa huduma kwa ukaribu zaidi, hivi sasa wanatambua umuhimu wa kusajili biashara zao kwani itawasaidia kuondosha usumbufu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Aidha wamesema kupitia elimu inayotolewa na BRELA inawaongezea uelewa wa kutanua shughuli zao za biashara ndani na nje ya nchi kwani wamekuwa wakitambuliwa kimataifa kupitia majina ya biashara au kampuni zao.
Sanjari na hayo wamesema kuwa usajili wa biashara kwa njia ya mtandao imekuwa huduma rahisi, kwani kunamuwezesha mteja kupata cheti chake papo kwa papo hasa kwa wale waishio vijijini na kuondoa usumbufu wa kuzifuata huduma za usajili katika ofisi za BRELA zilizopo Mjini.
No comments
Post a Comment