China na Urusi zapinga vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini
China na Urusi zimetumia kura za turufu kupinga azimio la Umoja wa Mataifa juu ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini.
Azimio hilo lilikuwa na lengo la kuiwekea nchi hiyo vikwazo vipya vikali zaidi baada ya kufanya majaribio kadhaa ya makombora ya masafa marefu yanayoweza kubeba mabomu ya nyuklia. Wajumbe 13 walipiga kura kuliunga mkono azimio hilo.
Urusi na China zimesema zinapinga vikwazo zaidi na zimesisitiza kuwa kinachohitajika sasa ni mazungumzo mengine baina ya Korea Kaskazini na Marekani.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini mnamo mwaka 2006 baada ya nchi hiyo kufanya jaribio la kwanza la silaha za nyuklia.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield ameelezea masikitiko yake juu ya kura za China na Urusi na amesema majaribio ya makombora ya masafa marefu yaliyofanywa na Korea Kaskazini mnamo mwaka huu ni tishio kubwa kwa usalama wa dunia.
No comments
Post a Comment