Header Ads

Header ADS

Clatous Chama kurudi nyumbani kwao Zambia


 Kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama hatokuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kesho Jumamosi (Mei 28), kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans.

Miamba hiyo ya Soka la Bongo itakuatana Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuanzia saa tisa alasiri, huku kila upande ukitamani kutinga hatua ya Fainali, na baadae kutawazwa kuwa Bingwa wa ‘ASFC’ msimu huu 2021/22.

Simba SC imethibitisha taarifa za Chama kuondolewa kwenye mpango wa kutumika kwenye mchezo dhidi ya Young Africans, kufuatia taarifa iliyotolewa kupitia Simba App.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Chama amerudishwa jijini Dar es salaam, na baadae atarejea nchini kwao Zambia kwa ajili ya kushiriki mwaka mmoja wa kifo cha Mke wake aliyefariki dunia Mei 28, 2021.

Chama alienda Mwanza akiwa na matumaini ya kucheza mchezo dhidi ya Young Africans, lakini hakuwa fiti baada ya kupata majeraha siku kadhaa zilizopita.

No comments

Powered by Blogger.