CHUO KIKUU CHA IBADAN NIGERIA CHAONESHA UTAYARI WA KUSHIRIKIANA NA VYUO VYA TANZANIA KUFUNDISHA KISWAHILI
Chuo kikuu cha Ibadan, Nigeria, kimeonesha utayari wa kushirikiana na vyuo vya Tanzania katika kufundisha Kiswahili. Dhamila hiyo imebainishwa wakati wa ziara ya Mhe Balozi Benson Alfred Bana chuoni hapo, tarehe 10 Mei 2022.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Balozi alifanya ziara hiyo kuushukuru Uongozi wa Chuo Kikuu cha Ibadan kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima Mwl. Julius Kambarage Nyerere nwaka 1979, ikiwa ni kutambua mchango wa Mwalimu katika mambo mbalimbali pamoja na ukombozi wa Bara la Afrika, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 100 ya Mwl. Nyerere.
Aidha, ziara hiyo imeweka msingi wa kujadili na kuona namna chuo hicho kinavyoweza kuanzisha ushirikiano na vyuo vya Tanzania hasa katika kufundisha somo la Kiswahili.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Ibadan, Prof. Kayode Adebowale alimshukuru Balozi Bana kwa ziara hiyo na akahidi kuwa chuo cha Ibadan kipo tayari kwa namna yoyote ile kushirikiana na vyuo vya Tanzania katika kufundisha Kiswahili pamoja na masuala mengine.
No comments
Post a Comment