Header Ads

Header ADS

Mama ajifungua Mtoto mwenye vichwa viwili

 Wanandoa kutoka eneo la Emoloi, Teso Kusini, katika Kaunti ya Busia nchini Kenya wanafadhaika baada ya mama kujifungua mtoto mwenye vichwa viwili.

Mama huyo, Nancy Apoma mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mama wa watoto wawili, anasema alijifungua mtoto huyo katika Hospitali ya Alupe.

 Punde alijifungua, aligundua kuwa mtoto huyo alikuwa na uvimbe mkubwa lakini kutokana na kukosa fedha aliruhusiwa kuenda nyumbani bila kujua kiini cha ugonjwa huo.

“Nilijifungua mtoto Given Aramisi katika Hospitali ya Alupe wiki tatu zilizopita. Mtoto wangu ana vichwa ‘viwili’ na aliruhusiwa kuondoka hospitalini kabla ya mtu yeyote kunieleza tatizo, sababu yake na tiba yake,” alisema.

Apoma alisema kipindi chote cha ujauzito wake, hakuwa na matatizo yoyote na alikuwa akienda kliniki kila mwezi. “Ultrasounds zilifanywa na walinihakikishia kuwa mtoto yuko katika hali ya kawaida na yuko katika hali nzuri zaidi ya kunipa dawa na vidonge vya madini ya chuma, ambavyo nilikuwa natumia. Kwa kweli sijui jinsi hii ilifanyika," alieleza 



No comments

Powered by Blogger.