Header Ads

Header ADS

Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Tabora

        Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora imewahukumu wa watu wanne wakazi wa nzega mjini kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la mauaji.
      Hukumu hiyo ya mauaji imetolewa  katika kikao cha Mahakama kuu kinachoendelea wilayani nzega mkoani Tabora ,Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda hiyo ,Amor Khamis amesema kutokana na ushahidi usioacha shaka uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo kuu imewakuta na hatia ya kuuwa .
Amesma kwamba ushaidi ulitolewa kwenye kikao hicho kinawatia  hatiani washitakiwa wote wanne pasipo shaka yoyote hivyo watakuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Jaji Khamis, alisisitiza jamii kuachana na dhamna ya ushirikina na kujipatia mali kwa njia ya mkato kitendo alichafanyiwa mwanafunzi huyo cha kumkata kichwa chake na kuondoka nacho kinatia simazi kwa jamii na familia Husika .
Awali wakili wa serikali kutoka ofisi ya Taifa ya mashitaka  wilayani nzega, ukiongozwa na Jenifa Mandago waliiambia  mahakama hiyo kuwa kati ya Tarehe 30 Septemba na Octoba 1 mwaka 2015 huko katika eneo la kijiji cha Silimka kata ya Utwigu wilaya ya Nzega na mkoa wa Tabora watu hao wanne wakiwa ni Samweli Maganga,Selemeni Saidi,Paulo Maganga na Juma dorard walimuuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Nzega , Hosamu Abdulhamani  kwa kutumia kitu chenye ncha kali ambapo walikitenganisha kichwa cha marehemu huyo na kiwiliwili chake.


No comments

Powered by Blogger.