Mji wa Donbas umeharibiwa kabisa, Zelensky anasema
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Urusi kwa kugeuza eneo la mashariki la Donbas kuwa ‘’kuzimu,’’ huku mapigano makali yakiendelea huko.
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya usiku kutoka Kyiv, alisema vikosi vya Urusi vimesambaratisha eneo hilo.
‘’[Kuna] mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo la Odesa, katika miji ya katikati mwa Ukraine. Donbas imeharibiwa kabisa,’’ alisema.
‘’Haya yote hayana na hayawezi kuwa na maelezo yoyote ya kijeshi kwa Urusi,’’ Zelensky aliongeza.
‘’Hili ni jaribio la kimakusudi na la uhalifu la kuua Waukraine wengi iwezekanavyo.
‘’Haribuni nyumba nyingi, vituo vya kijamii na biashara kadiri inavyowezekana,’’ kiongozi wa Ukraine alisema.
Siku ya Alhamisi, wizara ya ulinzi ya Ukraine iliishutumu Urusi kwa kuzidisha mashambulizi yake huko Donbas na kuwazuia raia kukimbia.
No comments
Post a Comment