Wabunge wa Umoja wa Ulaya wataka vikwazo dhidi ya kansela wa zamani wa Ujerumani Schröder
Wamesema Schoeder, mpaka sasa anakataa kuachana na marupurupu manono yanayotokana na kuwa kwake mjumbe wa bodi wa kampuni za nishati za Urusi. Hata hivyo azimio lililopitishwa halina meno ya kisheria licha ya kuungwa mkono kwa kiwango kikubwa na bunge linalolenga shabaha ya kuimarisha jibu kali dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Licha ya malamiliko makubwa nchini Ujerumani, Schroeder amekataa kabisaa kujiuzulu nyadhifa zake katika makampuni ya nishati ya Urusi ya Rosneft na Gazprom. Azimio la bunge la Ulaya linamtaka Schroeder kufuata nyayo za wengine kama waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa Francois Fillon ambaye ameshajitenga na kampuni za Urusi.
Kansela wa sasa wa Ujerumani Olaf Scholz anayetoka kwenye chama kimoja cha kisiasa na bwana Schröder cha SPD pia amemtaka kansela huyo wa zamani Gerhard Schröder ajitenge na kampuni za Urusi.
No comments
Post a Comment