Kherson kuwa sehemu ya Urusi, gavana mpya asema
Gavana aliyewekwa mamlakani na Urusi katika jimbo la kusini mwa Ukraine la Kherson amesema kuwa jimbo hilo hivi karibuni litaingizwa kikamilifu ndani ya Ukraine.
Volodymyr Saldo, ambaye aliwekwa mamlakani na vikosi vya Urusi baada ya kuchukua udhibiti wa eneo hilo mapema mwezi Machi, aliandika kwenye Telegram kwamba litakuwa “jimbo la Kherson la shirikisho la Urusi”.
Naibu wake, Kirill Stremousov, aliandika kuwa wakazi wa jimbo hilo wataweza kuwasilisha maombi ya uraia wa Urusi katika wiki zijazo wakati hali itakapoimarika.
Maafisa wa Ukraine wamekuwa wakionya mara kwa mara kwamba Moscow inapanga kuendesha kura ya maoni bandia katika jimbo hilo na maeneo mengine.
Hatahivyo, maafisa wa Urusi bado hawajathibitisha iwapo majimbo ya kusini mwa Ukraine yametwaliwa na msemaji Kremlin Dmitry Peskov alisema mapema mwezi huu kwamba hali ya baadaye ya maeneo hayo itategemea utashi wa wakazi.
No comments
Post a Comment