OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA YAMPOKEA KATIBU MPYA
Katibu wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Hassan Omani Kitenge ameripoti katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.
Bw.Kitenge amechukua nafasi ya Bw Xavier Daudi ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo Katibu kitenge amesema kuwa jukumu kubwa la Taasisi ni kuajiri na imebeba dhamana kubwa katika utumishi wa umma.
Aidha, Bw.Kitenge amesema maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ni kupata watumishi wa umma wenye uadilifu,wenye sifa na wenye kuwajibika kwa hiari ambao ndio watakaosukuma gurudumu la nchi kwenda mbele.
Bw.Kitenge amewataka watumishi hao kuchapa kazi kwa bidi na kumpa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kuyafikia maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kabla ya uteuzi Bw.Kitenge alikuwa Mkurugenzi wa Mikataba ya Utendaji kazi Serikalini, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
No comments
Post a Comment