Mkude na Chama kuikosa Azam FC Kesho
Viungo wa klabu ya simba, Jonas Mkude na Clatous Chotta Chama wamekosa mazoezi ya mwisho ya kikosi cha Simba SC kuelekea mchezo wa Mzunguko wa 24 wa Ligi Kuu Tanzania Bara ,NBC dhidi ya wana lambalamba Azam FC, utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam.
Simba SC imefanya mazoezi yake ya mwisho katika Uwanja wa Uhuru leo Jumanne (Mei 17) asubuhi, chini ya maafisa wote wa Benchi la Ufundi, ambalo linaongozwa na Kocha kutoka nchini Hispania Franco Pablo Martin.
Miamba hiyo itakutana kesho Jumatano (Mei 18) kuanzia mishale ya saa moja usiku, huku kila upande ukihitaji alama tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mapambano ya Ligi Kuu inayoelekea ukingoni.
No comments
Post a Comment