Mshukiwa wa mauji ya Rwanda Munyarugarama athibitishwa kufa
Mahakama hiyo imesema kwamba iligundua kuwa Phénéas Munyarugarama alifariki mwaka 2002 mashariki mwa jamuhuri ya Kidemokrasi ya Conge.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano , mahakama hiyo ilisema kuwa iliweza kubaini kifo chake ’’baada ya uchunguzi wa kina na wenye changamoto’’, na kwamba alikufa kifo cha kawaida tarehe 28 Februari 2002”.
Munyarugarama, ambaye ni kamanda wa zamani wa jeshi, amekuwa akishitakiwa mashitaka manane yakiwemo mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu.
"Kwa awaathiriwa na manusura wa uhalifu uliotekelezwa na Munyarugarama katika eneo la Bugesera, tunamatumaini matokeo haya yanafunga kesi ,"mwendesha mashitaka Serge Brammertz amesema katika taarifa.
Tangazo la hivi karibuni linafuatia tangazo lingine la mahakama la wiki iliyopita la kuthibitisha kifo cha mshukiwa Protais Mpiranyi ambaye pia alikuwa miongoni mwa washukiwa wakuu wanaosakwa na mahakama kwa mauaji ya Rwanda.
Takriban watu laki 800,000 waliuliwa kikatili na Wahutu wenye itikadi nchini Rwanda , katika kipindi cha siku 100 katika mwaka 1994.
Walikuwa wakiwalengawatu wa jamii ya Watutsi walio wachache pamoja na wapinzani wao kisiasa, bila kujali asili asili yao.
No comments
Post a Comment