Urusi inasema zaidi ya wapiganaji wa zaidi ya 900 wamepelekwa katika kambi ya jela
Zaidi ya wapiganaji 900 wa Ukraine ambao walikuwa wamekwama katika kiwanda cha chuma wa Azovstal katika Mariupol wamepelekwa katika kambi ya gereza katika eneo linalodhibitiwa na Warusi, imesema Moscow .
Urusi iliwaamrisha wanajeshi pale kujisalimisha kama sehemu ya mkataba uliofikiwa na pande zote, kama njia ya kuyaokoa maisha yao. Inaripotiwa kuwa kulikuwa na uhaba wa chakula na maji katika kiwanda hicho kwa wiki kadhaa.
Msemaji wa Wizara ya mambo yan je ya Urusi , Maria Zakharova, alisema Jumatano kwamba wanajeshi 959 walikuwa wamejisalimisha kwa Urusi tangu Jumanne . Kati ya wanajeshi hayo 521, walikuwa wanatibiwa majeraha na waliosalia wamepelekwa katika kambi ya zamani ya jela katika mji wa Olenivka katika eneo linalodhibitiwa lililopo katika jimbo la Donetsk.
Wizara ya ulinzi katika Kyiv ilisema kuwa inamatumaini kuwa kutakuwa na "utaratibu wa kubadilishana …kuwahamisha mashujaa hawa wa Ukraine haraka iwezekanavyo", kulingana na Shirika la habari la AFP.
Hatma yao imesalia kuwa haijulikani , huku msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov akikataa kusema iwapo watachukuliwa kama wahalifu au wafungwa wa kisiasa.
Wizara ya ulinzi ya Ukraine iliahidi kufanya "kila liwezekanalo" kuwaokoa wale ambao bado wamejificha kwenye mitandao ya mahandaki chini ya kiwanda cha chuma, lakini ilikiri kuwa hakuna njia nyingine ya kijeshi iliyopo ya kukwepa.
No comments
Post a Comment