Mwanaume Denmark ahukumiwa kifo
Raia mmoja wa Denmark amehukumiwa kifo nchini Nigeria baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mkewe na mtoto wao wa kike wa miaka mitatu.
Mahakama mjini Lagos imesema mwendesha mashtaka amewasilisha ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mtu huyo ambaye amehukumiwa kunyongwa. Mshtakiwa alikana kuhusika na mauaji hayo wakati kesi zikiendelea mahakamani.
Mauaji hayo yalifanyika mnamo Aprili 5, mwaka 2018 katika nyumba ya wanandoa hao katika kitongoji tajiri cha Banana Island cha Lagos.
Kesi hiyo iliibua hisia ya umma, haswa kutoka kwa makundi ya kutetea haki za wanawake. Hukumu ya kifo kwa kunyongwa ndio adhabu kuu kwa kosa la mauaji huko Nigeria, nchi ya Afrika Magharibi yenye watu milioni 212.

No comments
Post a Comment