Rais wa Marekani aonya juu ya uwezekano wa kuenea kwa homa ya nyani
Rais wa Marekani Joe Biden amesema leo Jumapili kwamba, watu wanapaswa kuwa waangalifu dhidi ya ugonjwa wa homa ya nyani ambao unaweza kuwa na athari kubwa ikiwa utaeenea zaidi.
Visa kadhaa vimegunduliwa Marekani na Ulaya mapema mwezi huu na kuzusha wasiwasi. Biden aliyeondoka leo Korea Kusini na kuelekea Japan, amesema wanashughulikia kikamilifu swala hilo na kutathmini aina ya chanjo dhidi ya virusi hivyo.
Watu wengi hupona katika wiki kadhaa baada ya kuambukizwa homa ya nyani.
Shirika la Afya duniani limesema kufikia jana Jumamosi kulikuwa na visa 92 vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo katika nchi ambazo si kawaida kukutana na ugonjwa huo.
No comments
Post a Comment