Mzozo kati ya Ukraine na Urusi kusababisha baa la njaa duniani - UN
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine huenda ukasababisha baa la njaa kote duniani katika kipindi cha miezi michache ijayo, Umoja wa Mataifa umeonya.
Katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres alisema kwamba vita hivyo vimesababisha ukosefu a usalama wa chakula katika mataifa masikini kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.
Dunia huenda ikakabiliwa na kiangazi kitakachochukua muda mrefu iwapo bidhaa za Ukraine hazitaimarishwa kwa kiwango cha kabla ya vita, aliongezea.
Mzozo huo umekata usambazaji wa bidhaa kutoka katika bandari za Ukraine, kama vile mafuta ya kupikia pamoja na nafaka kama vile mahindi na ngano.
Hali hiyo imepunguza usambaza wa bidhaa hizo hali iliofanya bei kupanda.Bei za vyakula duniani zinakaribia kupanda kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka uliopita , kulingana na Umoja wa Mataifa.
Akizungumza mjini New York siku ya Jumatano, bwana Guterres alisema kwamba mzozo huo unatishia kuwawacha bila chakula mamilioni ya watu na kusababisha utapiamlo, baa la njaa na kiangazi.
No comments
Post a Comment