Ndumbaro : atoa siku 30 kwa mawakili nchini kuwa na mihuri ya kielektoniki
Serikali imetoa siku 30 kwa mawakili wote kuhakikisha wanakuwa na mihuri mipya ya kielektoniki ili kuondoa malalamiko ya watu wanaojifanya mawakili (vishoka )kwa kutumia mihuri ya mawakili hao.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro wakati akifungua mkutano mkuu wa chama cha mawakili Tanzania (TLS) unaofanyika jijini Arusha.
Amesema kuwa, ni lazima ndani ya siku 30 mawakili wote lazima wawe na mihuri ya kielektoniki na baada ya hapo hawatatambua mihuri mingine yoyote ambayo sio wa kielektoniki.
“kwa miaka mingi kumekuwa na malalamiko ya watu kujifanya mawakili ambao wanafahamika kwa jina maarufu kama (vishoka) na kutumia mihuri ya mawakili hivyo naamini kupitia mihuri ya kieletroniki ambayo imeandaliwa na TLS ambayo nimeizindua leo itamaliza changamoto hiyo.”amesema Dokta Ndumbaro.
“ndani ya siku 30 lazima mawakili wote wawe na mihuri na tutaandikia mamlaka zote zinazotambua mihuri ya mawakili maelekezo ikiwemo TRA juu ya kuhakikisha mawakili wote wanakuwa na mihuri hiyo lengo likiwa ni kuondoa malalamiko ya watu wanaotumia mihuri ya mawakili.”ameongeza Dokta Ndumbaro.
Kwa upande wake Raisi wa chama cha mawakili Tanzania (TLS) Dkt. Edward Hosea amesema kuwa mkutano huo umewakutanisha mawakili wote kutoka Tanzania ambao ni wanachama.
Amesema kuwa,kutakuwa na mada tofauti zitakazowasilishwa na mawakili na kwamba wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kushirikiana na serikali ili waweze kutimiza majukumu yao kama nchi.
Dokt Hosea ameongeza kuwa, wamekuwa wakifanya mkutano huo kila mwaka na wanatarajia kujadili mada ambazo zitaleta tija na ufanisi katika chama hicho.
Hata hivyo katika mkutano huo waziri Ndumbaro ameweza kizindua mihuri ya kielektoniki,na kizindua Saccos ya mawakili.
Naye Captain Ibrahimu Bendera akitoa maelezo ya mihuri hiyo amesema kuwa mihuri hiyo mipya itasaidia kuwadhibiti vishoka wote ambao walikuwa wanatumia mihuri ya kawaida kiholela pamoja na wale ambao walikuwa wanavunja sheria na maadili ya taaluma ya uwakili.
Amesema kuwa, ili kuthibiti uharibifu ambao sio sahihi wameona watumie mihuri hii ya kieletroniki ili kuwadhibiti vishoka hao ambapo amesema kuwa, muhuri huo ukigonga unaweza ukaonyesha taarifa zote za mgongaji ikiwemo ya kuwa ni wakili wawapi je ni wakili ambaye amesajiliwa na chama na je anafanyia kazi zake wapi.
“Sisi kama mawakili tumekubaliana na uamuzi wa wizara waliotoa wa kuhakikisha
ndani ya mwezi mmoja kila wakili ana tumia muhuri huo. “amesema.
No comments
Post a Comment