Tanzania yakubaliana na nchi za kusini mwa afrika kuunda mfuko wa kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeingia makubaliano na Nchi za Kusini mwa Afrika kuunda mfuko maalum kwa kila nchi wa kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu hususan tembo
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja(Mb) katika Kongamano la
Tembo wa Afrika lililofanyika leo katika Hifadhi ya Taifa Hwange nchini
Zimbabwe.
“Tumekubaliana
kwamba kuwepo na mfuko maalum kwa kila nchi ambao utakuwa mahsusi kwa ajili ya
kudhibiti wanyama wakali na waharibifu kama tembo na pia kuwezesha wananchi
wanufaike na rasilimali wanyama hao” Mhe. Masanja amefafanua.
Ameongeza kuwa
mfuko huo utakapoanzishwa utawanufaisha wananchi wanaoishi pembezoni mwa
hifadhi na waathirika wa wanyama hao wanaoumizwa au kuuawa kwa kuwezesha
kulipwa fidia .
Mhe. Masanja
amesema kuwa sambamba na hilo mkutano huo umelenga kuangalia namna jamii
zinazoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi kuangalia namna zinavyoweza
kushirikishwa katika kutunza rasilimali za wanyama hususan tembo.
Aidha, amesema
nchi hizo zimekubaliana zisiingiliwe katika maamuzi na nchi za Magharibi kwa
kuwa zenyewe ndio zinahusika katika kutunza wanyama hao na pia zinazoathirika
na changamoto za wanyama hao.
Kongamano hilo
limehudhuriwa na Mawaziri na Maafisa Waandamizi kutoka nchi za Botswana,
Namibia, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Eblate Mjingo (kulia) na Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Kay Kagaruki wakifuatilia Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika kwenye Hifadhi ya Hwange nchini Zimbabwe.
Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa akifungua rasmi Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika kwenye Hifadhi ya Hwange nchini Zimbabwe. Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akifuatilia hotuba.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Mawaziri kutoka Zambia na Botswana wakiagana na Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa (kushoto) baada ya kufungua rasmi Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika kwenye Hifadhi ya Hwange nchini Zimbabwe.
No comments
Post a Comment