WAKALA ya Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa) imewafukuza kazi watumishi watatu wa Kivuko cha Magogoni- Kigamboni, Dar es Salaam.

Taarifa ya ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Temesa iliwataja waliofukuzwa ni nahodha, fundi wa kivuko na baharia.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa umma, watumishi hao wamefukuzwa kazi kutokana na tukio la Mei 24, mwaka huu la kuchelewesha kwa makusudi kivuko upande wa Kigamboni na kusababisha usumbufu na taharuki kwa abiria wanaotumia kivuko hicho.