Header Ads

Header ADS

YANGA SC yatembelea kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi Shinyanga mjini

 

Klabu ya Yanga imetoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula, katika kituo cha kulea  watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye Ualbino cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila ndani ya jamii.

Klabu hiyo imetoa msaada huo ikiwa imeambatana na wachezaji wake, na imepiga kambi mkoani Shinyanga kwa ajili ya kujiandaa na Mchezo wao wa Nusu Fainali wa kombe la Azam, ambao utachezwa siku ya Jumamosi Jijini Mwanza dhidi ya Klabu ya Simba katika uwanja wa CCM Kirumba.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Group ambao ndiyo wafadhili wa Klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Said, akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula, anasema wamekuwa na utaratibu wa kurudisha fadhila ndani ya jamii, kila wanapopita katika mikoa mbalimbali na kutoa msaada kwa wahitaji.

“Msaada ambao tumeutoa kwa watoto hawa wenye ulemavu mbalimbali hapa Buhangija Shinyanga ni Juice, mafuta ya kujipaka, Sabuni za kipande, mafuta ya kupikia, Maharage, Biskuti, Mahindi Unga, Sukari, na Mchele,”amesema Said.

Naye Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara, ameupingeza Mkoa wa Shinyanga kwa kuwalinda watoto wenye ualbino, huku akiwaomba viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya kidini hapa chini, kutoa elimu kwa wananchi kutowanyanyapaa watu wenye ualbino, bali waishi nao vizuri na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameipongeza Klabu hiyo ya Yanga, kwa kutembelea kwenye kituo hicho cha Buhangija na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula jambo ambalo watapata mibaraka na kufanya vizuri katika michezo yao.

Aidha Mlezi Mkuu wa kituo hicho Mwalimu Fatuma Gilala, ametaja idadi ya watoto wenye ulemavu mbalimbali ambao wanalelewa kwenye kituo hicho cha Buhangija kuwa wapo 238, Viziwi 41, Wasioona 87, na wenye Ualbino 110.

 

 
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akionyesha Jezi ya Klabu ya Yanga aliyokabidhiwa na kuandikwa jina lake.
 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza katika kituo cha Buhangija Jumuishi cha kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye Ualbino.

Mkurugenzi wa uwekezaji GSM kwa Klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Said akizungumza katika kituo hicho cha Buhangija Jumuishi wakati wa kukabidhi misaada mbalimbali kituoni hapo.

Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara akizungumza katika kituo hicho cha Buhangija Jumuishi wakati wa kukabidhi misaada mbalimbali kituoni hapo.

Mlezi Mkuu wa kituo hicho cha Buhangija Jumuishi Mwalimu Fatuma Gilala, akitoa shukrani kwa msaada huo kutoka Klabu ya Yanga.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Group Mhandisi Hersi Said akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye Ualbino katika kituo cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga.

Misaada mbalimbali ikikabidhiwa.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Group Mhandisi Hersi Said, (kushoto) akimkabidhi misaada mbalimbali Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko kwa ajili ya watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye Ualbino katika kituo cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga, (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Group Mhandisi Hersi Said, (kushoto) akimkabidhi misaada mbalimbali Afisa Elimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga, kwa ajili ya watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye Ualbino katika kituo cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said (katikati) wakimkabidhi mlezi Mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi Mwalimu Fatuma Gilala kwa ajili ya watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye Ualbino.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akionyesha Jezi ya Klabu ya Yanga iliyoandikwa jina lake.

Wachezaji wa Yanga wakiwa katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye Ualbino cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga, kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali.

Wachezaji wa Yanga wakiwa katika kituo cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga.
Wachezaji wa Yanga wakiwa katika kituo cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga.

Wachezaji wa Yanga wakiwa katika kituo cha Buhangija Jumuishi Mjini Shinyanga.

.

Watoto wakiwa kituoni wakipokea misaada kutoka Klabu ya Yanga.



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, wakipiga picha ya pamoja na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Fiston Mayele.


No comments

Powered by Blogger.