Polisi watumia gesi kuwatawanya waandamanaji Ufaransa
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwarudisha nyuma waandamanaji waliovalia mavazi meusi ambao walivamia majengo ya biashara mjini Paris siku ya Jumapili wakati wa maandamano ya Mei Mosi wakipinga sera za Rais mpya aliyechaguliwa tena Emmanuel Macron.
Maelfu ya watu walijiunga na maandamano hayo ya Mei Mosi kote Ufaransa wakitoa wito wa nyongeza ya mishahara, na kwa Macron kuacha mpango wake wa kuongeza umri wa kustaafu.
Maelfu ya watu walijiunga na maandamano hayo ya Mei Mosi kote Ufaransa wakitoa wito wa nyongeza ya mishahara, na kwa Macron kuacha mpango wake wa kuongeza umri wa kustaafu.
Waandamanaji wengi walifanya maandamano ya Amani lakini ghasia zilizuka katika mji mkuu, ambako polisi waliwakamata watu 54 akiwemo mwanamke ambaye alimshambulia mfanyakazi wa zimamoto aliyekwua anajaribu kuzima moto waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa Gerald Darmanin alisema kwenye Twitter. Polisi wanane walijeruhiwa aliongeza.
Makabiliano na polisi yalizuka mwanzoni mwa maandamano karibu na La Republique Square na hadi yalipofika La Nation Square huko mashariki mwa Paris.
Makabiliano na polisi yalizuka mwanzoni mwa maandamano karibu na La Republique Square na hadi yalipofika La Nation Square huko mashariki mwa Paris.
No comments
Post a Comment