Header Ads

Header ADS

Raia wa haiti wahama makazi yao kufuatia mapigano port- au -prince

 Raia wa haiti katika Mji Mkuu wa nchi hiyo Port-Au-Prince hapo jana waliyakimbia makaazi yao baada ya makabiliano ya risasi kuibuka kati ya makundi hasimu ya uhalifu. Haya ni kwa mujibu wa mashuhuda shilika la habari la Reuter.

Milio ya risasi ilisikika katika mtaa wa mabnda wa Cite Soleil ambapo watu walionekana kuacha makaazi yao na kukimbia. Baadhi walioenakana wakikimbia na kuinua mikono yao ili wasishambuliwe. Makabiliano kati ya makundi ya wahalifu yaliyojihami wiki iliyopita yalipelekea vifo vya karibu watu 20.

Mamlaka ya ulinzi wa raia ya Haiti imesema mapambano hayo yalikuwa kati ya kundi linalojiita Chen Mechan na jengine kwa jina 400 Mawozo ambalo lilihusika katika utekaji nyara wa wamishonari wa Kimarekani na Canada mnamo mwezi Oktoba. 

No comments

Powered by Blogger.