Header Ads

Header ADS

Tanroad Mkoa wa Songwe waendelea kufanya matengenezo ya Barabara

 Serikali ya Mkoani Songwe imesema imejipangakutatua adhaa ya watoto wa shule kusimama masomo kutokana na barabara kufungwa baada ya maporomoko makubwa ya vifusi vya milima katika kata ya Sange wilaya ya Ileje yaliyosabibishwa na mvua kubwa.                                
Hayo yamesemwa na mkuu  wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba alipofika katika kata za Sange na Ngulugulu kutembelea familia mbili zilizopata majanga  ya kupotelewa watu watano kutokana na nyumba zao kubomokewa na kufukiwa na vifusi vya udongo. 

 Alisema kutokana na barabara hiyo inayounganisha wilaya ya ileje na wilaya za mkoa jirani  wa Mbeya ambazo ni Rungwe na Kyela kuwa mawasiliano yamekatika hivyo kupelekea wananchi kushindwa kufika kupata huduma muhimu. 
       "Wakala wa barabara Tanroad mkoa wa Songwe wanaendelea na kufanya matengenezo ikiwa ni pamoja kutoa vifusi vyote vilivyopolomoka na kufukia barabara na kupelekea watoto kusimama masomo , huku mawasiliano pia yakikatika kati ya wananchi wa kata ya Sange kushindwa kusafiri kupatavhuduma ndani ya wilaya ya Ileje , mkoa wa Songwe na mkoa wa Mbeya ambako hupata huduma zao muhimu" alisema mkuu wa Mkoa.  
     Mkuu wa mkoa Aliwataka wananchi wa kata za Sange na Ngulugulu ambako kuna miinuko mingi  kupunguza magema ya udongo wakati wanajenga nyumba zao ili kuepukana na adhaa ya kufukiwa na udongo pindi mvua zinaponyesha kwa wingi kipindi cha mvua nyingi katika maeneo hayo.  
   Mwenyekiti wa kijiji cha Sange Fanikiwa Mbwile alisema mvua nyingi ambazo zinanyesha eneo hilo april 28 usiku zilisababisha maafa makubwa ya vifus vya milima kubomoka na kufukia nyumba mbili na kusababisha vifo vya familia mbili kufukiwa na udongo            akiwemo mama mjamzito na mtoto wa miaka mitano.                                      
 "Toka aprili 28 watoto wa shule mbili  ,Shule ya Msingi Sange na  shule ya Msingi Msalala wamesimama masomo kutokana na barabara  kufunikwa na udongo ulio poromoka kutoka milimani, walimu wamesimamisha masomo kwa muda wakati wakisubiri serikari kutoa vifusi kwa ajili ya usalama wa watoto wadogo kuanzia chekechea mpaka darasa la saba   ,pia hakuna mawasiliano ndani ya wilaya ya ileje na wilaya za mkoa jirani wa Mbeya ambako tunapata mahitaji yetu muhimu" alisema Mbwile                                     
Kwa upande wake Sifa Kibona  Mzazi wa mtoto awali katika shule ya Msingi Sange alisema wanawashukuru walimu kwa kusimamisha masomo kwa muda ili kuwanusuru watoto kusombwa na maji kutokana na barabara kufunikwa na vifusi vya udongo .   
Kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe,Janeth Magomi, alisema  kuwa watu watano waliofariki chanzo  kilikuwa ni kupasuka kwa sehemu ya mlima na kusabisha maporomoko yaliyoenda kufunika nyumba hizo ambazo marehemu walikuwa wamelala.
 "Matukio hayo yalitokea siku ya Aprili 28,   mwaka huu majira ya saa tisa alifajiri katika kitongoji cha Mjuni  kata ya Sange, Tarafa ya Bundari ,Wilayani Ileje na kusababisha vifo vya watu watatu wa familia moja kiwamo mtoto wa miaka mitano na mama mjamzito wakiwa wamelala 
" alisema.            
               
Kamanda Magomi aliwataja watu hao wa familia  waliofariki kuwa ni Lazaro Shibanda (22),Romania Kijalo (22), pamoja na Mtoto mdogo Ayub Shibanda(5).
Alisema tukio la pili ni la watu wengine wawili wa familia moja kufariki dunia ambalo lilitokea siku hiyo hiyo katika kijiji cha Kisyesye   Wilayani humo.
Aliwataja marehemu hao kuwa ni Eliud Kajange (26),pamoja na  mkewe Faraja Kajange (18).
Kutokana na barabara kukata mawasiliano Msafara wa mkuu wa mkoa akiambatana na mkuu wa wilaya ya Ileje Anna Gidarya walilazimika kuacha magari njiani na kutembea takribani kilomita saba kando kando ya milima kufuata familia zilizopata Maafa na kufikia ofis za kata hiyo.


No comments

Powered by Blogger.