RC MAKALLA: operesheni imedhibiti matukio ya panya road dsm.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amesema kufuata kuanzishwa kwa Operesheni kabambe ya kuwakamata Panya road waliokuwa wakifanya matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali ya Mkoa huo kwa sasa hali ya mkoa huo Shwari.
Mhe. Makalla amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwashughulikia kikamilifu Panya road huku akisema Watuhumiwa 35 wamefikiahwa Mahakamani, 17 Uchunguzi unaendelea.
RC Makalla amesema Mpaka Sasa Operesheni imefanikiwa kuwafikisha Mahakama Watuhumiwa 35 na wengine 17 wanaendelea kufanyiwa Uchunguzi.
Kutokana na hilo RC Makalla amewatoa hofu Wananchi wa Mkoa huo na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kuvunja Uti wa mgongo wa mtandao mzima wa Panya road.
Ili kuhakikisha matukio Kama hayo hayajirudii Mara kwa Mara, RC Makalla amesema wameweka Mpango mkakati endelevu kwa kudhibiti uhalifu wa aina yoyote usitokee kwenye Mkoa huo.
No comments
Post a Comment