RC NJOMBE AZINDUA AWAMU YA PILI YA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO
Tanzania ni moja ya mataifa yaliyokuwa yamejiweka bayana kufanikiwa kudhiti ugonjwa wa polio kwa muda mrefu lakini imelazimika kuanza kuchukua hatua za tahadhari kwa kuchanja watoto kufuatia nchi jirani ya Malawi yenye muingiliano mkubwa nasi kuripoti kisa kimoja februari 17 mwaka huu.
Katika uzinduzi uliyofanyika katika kituo cha afya cha Njombe mjini kimkoa ,Mkuu wa mkoa huo Waziri Kindamba amesema mkoa huo umechukua hatua za haraka kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo kwa kukamilisha chanjo ya awamu ya kwanza na kuanza awamu ya pili ,kati ya nne zitakazotolewa kwa watoto, kwasababu upo kwenye hatari zaidi ya kuathirika kutokana na kupakana zaidi na Malawi kupitia Ludewa.
Jambo la Kustaajabisha zaidi katika uzinduzi huo ,Akina baba wamejitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao kupata chanjo ambapo wanasema wamehamasika kufanya hivyo ili kuziweka familia zao katika hali ya usalama kiafya.
Wakati serikali ikifanya jitihada kulinda watu wake ,Shirika la kuzuia magonjwa duniani CDC kupitia kwa msimamizi wa chanjo mkoa wa Njombe Dr Monica Mwengee anaeleza mikakati iliyowekwa ili kuzuia mlipuko huo ikiwa ni pamoja na kuandaa vipeperushi huku kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Manyanza Mponeja akiweka bayana malengo ya mkoa ya kuchanja watoto waliyochini ya miaka mitano wapatao laki moja na kumi
Katika awamu ya kwanza Njombe ilifanikiwa kuchanja watoto wa chini ya miaka mitano kwa asilimia 116 huku katika awamu ya pili ukitarajia kuchanja watoto zaidi ya laki moja na kumi.
No comments
Post a Comment