Header Ads

Header ADS

Serikali kuboresha Mialo Ziwa Tanganyika

 Serikali imesema inafanya jitihada za kuupandisha hadhi mwalo wa wavuvi wa samaki wa Kirando uliopo Wilaya ya Nkasi ili uweze kufikia hadhi ya kuwa soko la kisasa la samaki na mazao ya uvuvi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega ameliambia bunge leo Jumatatu Mei 23, 2022 wakati akijibu swali la mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kujenga Soko la kisasa la mazao yatokanayo na uvuvi Wilayani Nkasi.

Ulega amesema mpango wa Serikali ni kujenga na kuboresha miundombinu ya uvuvi ikiwemo mialo na masoko katika maeneo mbalimbali nchini.
Ulega amesema kwa upande wa mwambao wa Ziwa Tanganyika unaojumuisha Wilaya ya Nkasi shughuli za uvuvi zinafanyika katika mialo ipatayo 239.
“Kati ya mialo hiyo, Serikali imeboresha mialo minne ya Kibirizi (Manispaa ya Kigoma ujiji), Ikola (Tanganyika), Muyobozi (Uvinza) na Wilaya ya Kirando (Nkasi),”amesema Ulega.
Waziri huyo amesema Serikali imejenga na kuboresha masoko mawili ya samaki ya Kibirizi (Kigoma) na Kasanga ambalo lipo katika wilaya ya Sumbawanga.
Kuhusu ulinzi wa mazalia ya samaki Naibu Waziri amesema ulinzi wa maeneo ya mazao ya samaki ni jukumu la kila mtu na kwamba hawatamfumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuhusika katika kuharibu maeneo ya mazalia.

No comments

Powered by Blogger.