Shaka atoa siku 7 kwa viongozi wa soko la Feri kumaliza changamoto zao
Katibu wa NEC, itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Shaka Hamdu Shaka, ametoa muda wa Siku Saba kwa Viongozi wa Soko la Samaki Feri pamoja na Wafanyabiashara katika eneo hilo kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kuangalia namna ya Kutatua Changamoto ambazo zipo kwenye Soko hilo la Samaki ambalo lipo Jijini Dar es Salaam.
Shaka ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2022 wakati wa ziara yake katika Soko hilo la Samaki Feri.
Akizungumza na Wafanyabishara wa Soko hilo la Samaki amewataka kuishi kwa kwa kuzingatia maono, Dira pamoja na uwajibikiaji ambao umekuwa ukisisitizwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
"Nataka niwaambie ndugu nimetoa Siku Saba ili mkae chini na mmalize changamoto zenu, kisha mtakayo kubaliana Myafikishe Serikali na Kwenye Ngazi za Chama cha Mapinduzi CCM" amesisitiza Shaka.
Kwa Upande wake mkuu wa Wilaya ya Ilala Ludigija Ng'wilabuzu amemueleza Katibu huyo wa NEC, Itikadi na Uenezi namna ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu imekuwa ikisogeza huduma za Kijamii kwa Wananchi ikiwemo Upatikanaji wa Maji Safi na Salama, huduma za Afya pamoja Uboreshaji wa Sekta ya Elimu.
"Pamoja na hayo Serikali imekuwa ikitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, imekuwa na mpango mzuri kwa ajili ya Wafanyabiashara ndogo ndogo kwa kuwawezesha kupata Fedha zinazotokana na Mikopo inayotolewa kupitia halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam" amesema Mkuu wa Wilaya Ludigija Ng'wilabuzu.
No comments
Post a Comment