Header Ads

Header ADS

Benki ya CRDB yatoa msaada wa vifaa vya studio kwa jeshi la zimamoto na uokoaji nchini



Benki ya CRDB imetoa msaada wa vifaa vya Studio na Tehama kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ikiwa ni kuliongezea nguvu Jeshi hilo katika utoaji wa taarifa mbalimbali na elimu kwa umma juu ya majanga ya moto nchini.
 

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo,
iliyofanyika kwenye Ofisi za Jeshi hiyo, Ilala jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili, alisema wamemeamua kulisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kurahisisha mawasiliano na kuwawezesha wananchi kufikiwa na taarifa zinazohusu maswala mbalimbali ya Zimamoto na Uokoaji popote na wanapokuwa na wakati wowote. 

Vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Kompyuta mbili aina ya iMac na Mac book Pro, Televisheni Hisense 55", Vifaa vya Studio pamoja na kamera aina Canon Mark IV 5D, vyote vikiwa ni vifaa vya kisasa kabisa ili kuendana na hali ya sasa katika teknolojia.

Akipokea Msaada huo, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Mbaraka Semwanza alisema msaada huo utakuwa chachu kwa wanahabari wa Jeshi kuhakikisha Elimu ya Kinga na Tahadhari inaufikia Umma kwa kiwango kikubwa tofauti na hapo awali.

Kamishna Semwanza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ameishukuru sana Benki ya CRDB, na kuahidi kuwa yale waliyoyakusudia kuyafanya yatafanyika kwa kiwango kikubwa sana na habari zitawafikia watu wengi tofauti na hapo awali.



Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki ta CRDB, Stephen Adili (wa tatu kulia) akimkabidhi Kamishna wa Utawala na Fedha Jeshi la Zimamoti, Mbaraka Semwanza (wa tatu kushoto), sehemu ya vifaa vya Studio na Tehama, vitakavyotumiwa na Jeshi la Zimamoto kutoa taarifa mbalimbali kwa Umma, katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye Ofisi za Jeshi hiyo, Ilala jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni Meneja Mwanadamizi wa Huduma Mbadala Benki ya CRDB, Mangire Kibanda, Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Farida Hamza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto, Puyo Nzalayamisi pamoja na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Ilala, Mrakibu Elisa Mugisha.
Kamishna wa Utawala na Fedha Jeshi la Zimamoti, Mbaraka Semwanza akijaribu moja ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Benki ya CRDB, vitakavyotumiwa na Jeshi la Zimamoto kutoa taarifa mbalimbali na elimu kwa umma juu ya majanga ya moto. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki ta CRDB, Stephen Adili.
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki ta CRDB, Stephen Adili akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya Studio na Tehama, vitakavyotumiwa na Jeshi la Zimamoto kutoa taarifa mbalimbali na elimu kwa umma juu ya majanga ya moto, iliyofanyika kwenye Ofisi za Jeshi hiyo, Ilala jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Kamishna wa Utawala na Fedha Jeshi la Zimamoti, Mbaraka Semwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto, Puyo Nzalayamisi pamoja na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Farida Hamza.
Kamishna wa Utawala na Fedha Jeshi la Zimamoti, Mbaraka Semwanza akizungumza wakati akitoa shukrani wa Benki ya CRDB, baada ya kupokea vifaa vya Studio na Tehama, vitakavyotumiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoa taarifa mbalimbali na elimu kwa umma juu ya majanga ya moto, katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Jeshi hiyo, Ilala jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.