Paris St-Germain itakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Brazil Neymar, 30, ikiwa watapata ofa inayokubalika msimu huu wa joto. (Goal)


Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig Mfaransa Christopher Nkunku, 24. (Goal)


The Blues wanaweza kufanya jaribio la dakika za mwisho kumnasa kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 22, mbele ya Real Madrid mara tu mchakato wa ununuzi wa klabu hiyo utakapokamilika. (Goal)


Tottenham wanamnyatia kiungo wa Italia na Inter Milan Alessandro Bastoni, 23, huku Manchester United pia wakionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Gazzetta dello Sport -kwa Kiitaliano)


Kipa Muingereza Fraser Forster, 34, amefanyiwa uchunguzi wa imatibabu huko Hotspur Way katika hatua ya kukamilisha uhamisho wake wa Spurs wakati mkataba wake wa Southampton utakapokamilika mwezi ujao. (Mail)


Arsenal wanamfuatilia kwa karibu mchezaji Alvaro Morata. Mshambuliaji huyo wa Uhispania, 29, amekuwa Juventus kwa mkopo wa msimju mzima jutoka Atletico Madrid. (Tuttosport -kwa Kiitaliano)


Mlengwa wa Tammy Abraham anasema 'anafurahia zaidi' kuwa Roma lakini mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa miaka 24 hajaweka bayana ikiwa atarejea kwa Ligi ya Mprimia msimu huu wa joto. (Metro)


Arsenal pia wanataka kumsajili tena winga wa Ujerumani Serge Gnabry kutoka Bayern Munich lakini hawana uwezo wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu huu wa joto. (Falk Christian)


Arsenal wametoa ofa ya mwisho kwa mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah mwenye umri wa miaka 22 - na kuna hisia kubwa kwamba atasaini kusalia zaidi ya mkataba wake wa sasa ambao unamalizika msimu wa joto. (Mail)


Aston Villa wako tayari kuongeza kasi ya kumsaka beki wa Rangers na Nigeria Calvin Bassey mwenye umri wa miaka 22. (Times)


Barcelona wamekutana na wakala wa kiungo wa kati wa klabu ya Villa na Uingereza wa chini ya umri wa miaka 19 Carney Chukwuemeka, 18. (Sport - kwa Kihispania)