Matokeo ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid yanaweza kuamua mshini wa mwaka huu wa tuzo ya Ballon d'Or, kulingana na mlinzi wa zamani wa Reds Djimi Traore.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa beki wa kushoto wakati klabu hiyo ya Anfield ilipotwaa kombe mwaka wa 2005 anadhani mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane yuko katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo - lakini anasema anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mshambuliaji wa Real na Ufaransa Karim Benzema.

Benzema, 34, amefung amabao 15 Ulaya msimu huu na kuwezesha miamba hao wa Uhispania kukutana na goals in Europe this Liverpool mjini Paris Jumamosi hii.

Mane alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa kwanza wa Senegal wa taji la Kombe la mataifa ya Afrika mwezi Februari na kusaidia Teranga Lions kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022, Huku nyota huyo wa miaka 30- akishindia klabu yake makombe mawili ya nyumba msimu huu.

"Nadhani Karim Benzema yuko katika hali nzuri maishani mwake - anafanya vyema," Traore aliiambia BBC Michezo Afrika.

"Nadhani mshindi wa Ligi ya Mabingwa, zawadi ya mtu binafsi itakuwa kama kushinda Ballon d'Or. Hivi sasa inaonekana itakuwa kati ya Benzema na Mane."

Walioteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu watatangazwa tarehe 12 Agosti, huku mshindi akitangazwa katika hafla itakayofanyika Paris mnamo Oktoba 17.

Waandalizi wa Soka ya Ufaransa wameamua kuwa zawadi hiyo sasa itaamuliwa kutokana na uchezaji wake katika msimu mmoja badala ya mwaka wa kalenda, ambao ulikuwa muundo wa awali.

Pambano la Jumamosi kati ya Real Madrid na Liverpool mjini Paris ni mechi ya marudiano ya fainali ya Ligi ya Mabingwa 2018, wakati Wahispania hao waliibuka washindi 3-1 na kutwaa taji lao la 13 la Uropa.