Header Ads

Header ADS

Viongozi 20 CHADEMA mkoani Manyara waachiwa huru

bavicha pic2

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) John Pambalu, Katibu Mwenezi, Twaha Mwaipaya pamoja na viongozi wengine 18 wa Chama hicho Wilaya ya Babati mkoani Manyara waliokuwa wamekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani humo wameachiwa kwa dhamana.

Viongozi hao walikamatwa wakidaiwa kufanya mikutano isiyo halali kwenye vijiwe mbalimbali mjini Babati wakitoa elimu ya kudai Katiba mpya.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa Manyara, Benjamin Kuzaga amethibitisha kuachiwa huru viongozi hao.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Babati, Edgar Mwageni amesema viongozi hao walikamatwa wakiwa wanazunguka kuzungumza na baadhi ya wanachama wao mjini Babati wakihamasisha juu ya kampeni yao ya kitaifa ya chama hicho ya "Join the Chain".

Mwageni amesema jana Jumanne walikaa kikao cha ndani katika Ukumbi wa AVIT mtaa wa mji mpya na kuzungumza juu ya umuhimu wa Katiba mpya bila usumbufu wowote.

"Haijulikani ni sababu ipi ilisababisha maofisa hao kukamatwa lakini huenda walikamatwa kwa sababu ya mkusanyiko usiokuwa na kibalii," amesema.

bavucha pic

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema Taifa (Bavicha), John Pambalu (watatu kulia) na Katibu Mwenezi Bavicha, Twaha Mwaipaya wapili (kushoto) wakiwa kwenye kijiwe cha kahawa na baadhi ya wakazi wa mjini Babati mkoani Manyara kwenye kampeni yao ya 'Join The Chain' kabla ya kukamatwa na Polisi.


BARUA ILIYOTOLEWA JANA NA CHADEMA 

ß    

 

No comments

Powered by Blogger.