ACT-Wazalendo waeleza haya kuhusu stakabadhi ghalani
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema hakitachoka kuzungumzia suala la stakhabadhi ghalani hadi pale serikali itakapofanya marekebisho ya mfumo ili kuleta unafuu kwa wakulima ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiulalamikia kuwa hauna manufaa kwao.
Stakabadhi ghalani ni mfumo wa kukusanya mazao pamoja kwenye ghala maalumu lililosajiliwa na Serikali kwa lengo la kuyauza kwa bei ya ushindani.
Katika mfumo huo, asasi za fedha zinaweza kutoa mkopo kwa dhamana ya mazao hayo yaliyohifadhiwa kwenye ghala na malipo ya wakulima yanafanywa baada ya mazao hayo kuuzwa.
Duni ametoa kauli leo Jumatatu Juni 20, 2022 wakati akizungumza na wanachama na wananchi wa majimbo ya Tunduru Kusini na Kaskazini mkoani Ruvuma.
Vikao hivyo ni mwendelezo wa mwenyekiti huyo kuimarisha chama hicho.
"Huu ni mfumo ni miongoni mwa mambo yanayonisumbua kwa sababu unawatesa na kuwanyanyasa wakulima wa maeneo mbalimbali sio mikoa ya kusini pekee. Sio jambo zuri kumpangia bei mkulima maana anapolima na kufanya palizi anapambana lakini akitaka kuuza ni ishu.”
"Mbona wakulima wa machungwa au karanga hawafanyiwi hivi ila korosho na mazao mengine ni stakabadhi ghalani tutafika kweli? Nataka niwaambie ACT itaendelea kulisemea hili hadi mfumo utakafanyiwa maboresho na marekebisho," amesema Duni.
Katibu
wa ACT- Wazalendo wa Mkoa wa kichama wa Selous, Abdallah Mtutura amemshukuru
Duni kwa kuzungumzia jambo hilo, akiungana na mwenyekiti wake akisema bado
linawatesa wakulima wakiwemo wa korosho wanaoulalamikia kwa nyakati.
No comments
Post a Comment