Lipumba akosoa vitambulisho vya Taifa kuunganishwa na ulipaji kodi
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Waziri wa Fedha na
Mipango, amefanya makosa ya kimkakati kuunganisha vitambulisho vya Taifa
na ulipaji wa kodi huku akieleza kuwa itaathiri motisha ya wananchi
kujisajili kupata vitambulisho hivyo.
Juni
14,2022 wakati waziri huyo akiwasilisha bajeti ya mwaka 2022/23, alisema
Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila
Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi kwa utaratibu wa usajili wa
namba ya utambulisho wa Taifa.
Amesema
hadi sasa Serikali haijakamilisha shughuli ya kuwapatia vitambulisho vya Taifa
Watanzania wote baada ya zaidi ya miaka kumi toka Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (Nida) kuanzishwa hivyo ni muhimu Serikali ikajikita kuharakisha
wananchi kupata vitambulisho vyao.
"Vitambulisho
vya kitaifa na teknolojia ya kielektroniki ni nyenzo ya kuongeza kasi ya
maendeleo. Ni makosa makubwa ya kimkakati hivi sasa kuunganisha vitambulisho
vya taifa na ulipaji wa kodi."
"Itaathiri
motisha ya wananchi kujisajili kupata vitambulisho vya kitaifa. Waziri wa fedha
anarejesha kinyemela kodi ya kichwa kupitia vitambulisho vya Taifa. Hili
halikubaliki. Utozaji wa kodi uambatane na uwezo wa kuilipa."
"Kasi
ya watu kujiandikisha kupata vitambulisho itapungua kwani kila mtu ataamini
akipata namba ya kitambulisho atakuwa analipa kodi," amesema
No comments
Post a Comment