CHADEMA yaitaka serikali kushusha bajeti kutoka trilioni 41
Chama cha Demokrasia na maendeleo ,CHADEMA, mhe, John kimeitaka serikali kushusha bajeti kutoka trilioni 41 ambayo wameiwasilisha badala yake itengeneze bajeti kwa kadri ya uzoefu na uhalisia wa ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Tamko hilo limetolewa na Katibu mkuu wa chama hicho, mhe, John Mnyika wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi ni
kasi ambayo hairidhishi,
“Kasi yetu ya ukuaji wa uchumi wan chi ni kasi
ambayo hairidhishi, kuna sekta muhimu zenye kugusa maisha ya wananchi
zinadondoka badala ya kuongezeka, hali ambayo inahitaji hatua za ziada za
serikali kuinusuru nchi na hali hii,” alisema Mnyika
“Hiki ambacho serikali imejivunia bungeni kwamba
kuna ukuaji wa uchumi kwa sababu tu la ongezeko la 0.1%, kutoka 4.8% mwaka 2020
mpaka 4.9% haistahili pongezi kwa serikali. serikali ieleze hatua zaidi ambazo
zitachukuliwa ili kuongeza kasi ya ukuaji uchumi.” Mnyika
Aidha alisema bajeti ya serikali ilitakiwa
kuindiza mradi wa katiba mpya na kupewa kipaumbele kwani ni mradi ambao taifa
lilishaanza miaka mingi hapo nyumamnamo mwaka 2014 na tayari nchi imeshatumia
mabilioni ya pesa.
Pamoja na hayo Mnyika amesema ripoti ya CAG ya
mwaka 2021 kama zilivyo kwenye ripoti za miaka ya nyuma zimeanisha ufisadi
mkubwa ndani ya serikali na ndani ya mashirika ya Umma, lakini hawajaona hatua
zozote bungeni wakati wizara mbalimbali zinajadiliwa.
Ameongeza kuwa wakati taifa linapitia katika
kipindi kigumu kiuchumi na wananchi wanapitia mazingira magumu serikali
inapaswa iwe ya utekelezaji.
“Katika mazingira ambayo taifa linapitia kwenye
hali ngumu kiuchumi na wananchi wanapita katika mazingira ya kufunga mkanda,
wakati umefika sasa serikali kutekeleza mapendekezo yetu ya muda mrefu wa
kupunguza ukubwa wa serikali” alisema Mnyika
“Bajeti ya serikali lazima ikizi vipaumbele na
matakwa ya wananchi kwa kuzingatia siyo tu mipango ya muda mrefu ya nchi bali
bajeti ya serikali lazima izingatie uhalisia wa matakwa na mahitaji ya wananchi ya wakati
huo bajeti inapitishwa”
Hatahivyo Alisema bunge halitekelezi majukumu
yake huku akigusia suala la tozo za kidi ya mafuta kemba haviguswa,
"Bunge
halitekelezi majukumu yake ya kuishauri na kuisimamia Serikali, michango inayoendelea
sasa haiangazii mapungufu na udhaifu wa bajeti." Mhe.
"Kwa takwimu za Serikali tozo na kodi za mafuta kwa
Petroli ni shilingi 920.68, Dizeli ni shilingi 813, mafuta ya taa ni shilingi
577. Eneo hili la kodi halijaguswa."Mhe Mnyika
No comments
Post a Comment