UWT Iringa yapongezwa ujenzi wa nyumba za makatibu
Umoja wa wanawake Tanzania
UWT mkoa wa Iringa umepewa pongezi kwa ujenzi wa nyumba za makatibu,
kukiimarisha chama na kuongeza ushirikiano baina ya serikali na chama cha
mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa.
Pongezi hizo zimetolewa na
mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudentia Kabaka wakati wa ziara yake ya siku mbili
ndani ya mkoa huo ambapo amesema uongozi wa umoja huo umefanikisha kukituliza
chama cha mapinduzi kutokana na utulivu uliopo kwenye jumuiya hiyo.
Kabaka alisema kuwa viongozi wa UWT mkoa wa Iringa
wamekuwa viongozi imara katika kuiongoza jumuiya hiyo ndio maana wamekuwa na
umoja na mshikamano katika uongozi.
Alisema kuwa kwa mara ya kwanza miaka mitano ya
uongozi wake amefanikisha kuongeza idadi ya wabunge wa viti maalum kuwa wengi
bungeni.
Kabaka alisema sasa ni wakati sahihi wa kuchagua
viongozi ambao wataweza kuiongoza jumuiya hiyo na kuendelea kuwa imara kwa
ustawi wa chama cha mapinduzi.
Aliongeza kuwa wanawake wote wenye sifa za
kugombea nafasi mbalimbali ndani ya jumuiya hiyo wachukue fomu na wagombee kwa
ajili ya kuingoza na kuikuza jumuiya hiyo.
Alisisitiza kwamba chama cha mapinduzi
kinautaratibu mzuri wa kuwachuja viongozi wanaotaka kugombea hivyo amewataka
kuondoa wasiwasi wa kugombea nafasi mbalimbali ndani ya UWT
Pia aliwashukuru kabila la wahehe kwa kumvisha
nguo za kihehe ambazo zimemuongezea heshima kubwa katika uongozi wake.
Alipovishwa mavazi ya kihehe alisema amefurahi
kuvishwa vazi hilo ambalo kwa miaka mingi amekuwa anaona kwenye tv tu historia
ya chief mkwawa hivyo ameahidi hata livua vazi hilo hadi amalize ziara mkoa wa
Iringa na ataendelea kulivaa mara kwa mara.
Lakini pia mwenyekiti wa UWT Taifa aliwashukuru
UWT mkoa wa Iringa kwa tuzo na zawadi mbalimbali ambazo amepewa leo mkoa wa
Iringa kuwa hatawasahau wema wao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa
Iringa,Niocolina Lulandala alisema kuwa wanampongeza mwenyekiti wa UWT Taifa
Gaudentia kabaka kwa kuijenga ofisi ya UWT ambayo idara zote za jumuiya hiyo
zinapatikana makao makuu ya chama jijini Dodoma hivyo kwa miaka yake mitano
amefanya maendeleo makubwa kwenye umoja huo.
Lulandala alisema mwenyekiti wa umoja huo
amefanikiwa kuunganisha jumuiya ya UWT kuwa na umoja na ushirikiano ambao umesaidia
kuongeza wanachama wapya na kukisaidia chama kufanya vizuri kwenye nyanja
mbalimbali za utawala.
Alisema kuwa wameendelea na ujenzi wa nyumba za
watumishi wa jumuiya ya UWT mkoa wa Iringa ambazo zitawasaidia kuacha kupanga
mtaani ili kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa UWT Taifa katika kuhakikisha
watumishi wote wanaishi kwenye nyumba zao
Pamoja na yote Mwenyekiti wa UWT Taifa amekabidhiwa
tuzo ya umahiri katika kuiongoza jumuiya ya UWT taifa kwa kuiwezesha jumuiya
hiyo kuwa na umoja na ushirikiano katika kukikuza chama cha mapinduzi.
Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga alisema
kuwa chama cha mapinduzi CCM Iringa wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na serikali
ndio maana mkoa wa Iringa umetulia na unafanya kazi za kimaendeleo.
alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa umetoa
zaidi ya bilioni kwenye mfuko wa akina mama wa asilimia 4 na wamejipanga
kuhakikisha mwaka ujao wa fedha wataongeza zaidi ya hapo.
Sendiga alisema kuwa serikali ya awamu ya sita
imefanikiwa kuwatua ndoo wanawake wa mkoa wa Iringa kwa kuleta miradi mingi ya
maji kila wilaya na halmashauri zake.
Alisema kuwa Iringa bado kunachamoto ya ukatili wa
kijinsia hivyo serikali ya mkoa wa Iringa imeanza kuwafunga watu wote ambao
wamekuwa wanafanya vitendo vya kikatilii.
Sendiga alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa
waache mara moja tabia ya kuwaficha wananchi ambao wamekuwa walifanya vitendo
vya ukatili wa kijinsia ili serikali ichukue hatua stahiki kwa watuhumiwa hao.
Mwenyekiti wa cham cha mapinduzi (CCM) mkoa wa
Iringa Dkt Abel Nyamahanga alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga
amekuwa kiongozi bora kuiongoza Iringa kuleta maendeleo ya wananchi.
Dkt Nyamahanga alisema kuwa chama cha mapinduzi
CCM mkoa wa Iringa kimemteua mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga kuwa balozi
wa kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia mkoa wa Iringa.
Aidha Dkt Nyamahanga alisema kuwa wanachama wote
wa CCM mkoa wa Iringa wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani
ya chama hicho bila uoga wowote ule.
Alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa itawachukulia
hatua kali watu wote ambao wameanza kampeni mapema na wale ambao wamekuwa
wakitoa na kupokea rushwa ili wapate uongozi.
Nyamahanga alisema kuwa Iringa wataendelea kuunga
mkono juhudi za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM taifa ambaye ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kila jambo
ambalo amekuwa akilifanya kuleta maendeleo kwa watanzania
No comments
Post a Comment