Jeshi la polisi mkoani Mbeya lakamata pombe zilizopigwa zilizokatazwa Tanzania
Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya
limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na pombe kali
zilizopigwa marufuku nchini.
Katika taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ulrich
Matei imesema ,mtuhumiwa huyo anafahamika kwa jina la Ishengoma Peter Kaswela (36)Mkazi
wa Ndandalo alikamatwa Mnamo tarehe 18.06.2022 majira ya saa 11:00
jioni, akiwa na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini zikitokea nchi jirani ya
Malawi ambazo ni Ice Dry London Gin box 01 na Coferhum box 05 ambazo ni
sawa na chupa 120.
Kamanda amesema alikamatwa wakati jeshi la polisi likiwa kwenye huko Kasumulu Kitongoji cha Seko, Kijiji na Kata ya
Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.
Aidha Matei amesema mtuhumiwa ni muingizaji wa
bidhaa za magendo na muuzaji wa pombe hizo.
Katika
hatua nyingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu katika
maeneo mawiwi tofauti wakiwa na Pombe haramu ya Moshi (Gongo).
Watuhumiwa
wawili wa kwanza ni Hawa Kapangala (40) mkazi wa Kiwira na Emanuel Edwin Mwakajela
(50) mkazi wa Kiwira ambao walikamatwa mnamo tarehe 17.06.2022 majira ya saaa 06:45 mchana
katika Kitongoji cha Kiwira kati, kijiji
cha Mpandapanda, kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe,wilayani Rungwe.
Pia katika
kitongoji cha Mshikamano, Kata ya Nsalala,
Tarafa ya Usongwe, Mkoa wa Mbeya mnamo 18.06.2022 majira ya saa 05:00 asubuhi, jeshi
la polisi lilifanikiwa kumkamata Yunice Geofrey Mwakifwamba [40] mkazi wa Mshikamano,
akiwa na Pombe Haramu ya Moshi lita 15 akiwa amehifadhi katika madumu mawili ya
lita 5 na chupa za maji nne zenye ujazo wa lita 1.5 zikiwa na kuzificha
uvunguni mwa kitanda.
Watuhumiwa wote ni wauzaji wa Pombe hiyo na watafikishwa mahakamani mara
baada ya upelelezi wa mashauri yao kukamilika.
No comments
Post a Comment