Header Ads

Header ADS

Adaiwa kumbaka mtoto kwa ahadi ya kulipwa ng’ombe watatu


Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Juma Jackson (30) mkazi wa Kijiji cha Kagunga wilayani Tanganyika akituhumiwa kumbaka na kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

mtuhumiwapic

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema mtuhumiwa alimvizia mtoto huyo akiwa anatoka nyumbani kwao kuelekea mji wa jirani.

"Alimvutia vichakani kisha kumvua nguo zake na kuanza kumbaka na kumlawiti huku akimkaba shingo na kumuamru asipige kelele," amesema Makame.

Hata hivyo, amedai kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina, aliahidiwa kulipwa ng'ombe watatu baada ya kutekeleza kitendo hicho na mtu (jina limehifadhiwa).

"Walikubaliana baada ya kufanya unyama huo aende akamuogeshe shambani kwake ili iwe kama zindiko kwa ajili ya shamba," amefafanua Makame.

"Tulimkamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa wazazi wa mtoto, alifanya ukatili huo Mei 13, 2022 saa 12:00 jioni, anaendelea kuhojiwa tukikamilisha upelelezi  tutamfikisha mahakamani," amesema Makame.

Wakati hayo ya kijili jeshi hilo pia linawashikilia  Kingi Gabriel (49), Masunga Peter na Simon Frederick wakazi wa Kijiji cha Ibindi halmashauri ya Nsimbo wakituhumiwa kupanga njama za kumuua Kelvin Isack.

Inadaiwa kuwa watu hao wote kwa pamoja walipanga njama za kumuua mlalamikaji Kelvin baada ya kumuonya Kingi Gabriel kuwa aachane na mke wake.

"Badala yake alikaidi na kuendelea kuwa na mahusiano naye na aliamua kupanga njama za kumuua mlalamikaji, tulipata taarifa tukawakamata na wanahojiwa kisha watafikishwa mahakamani," amesema Makame.

No comments

Powered by Blogger.