Viongozi wa CHADEMA waliokuwa nje sasa kurejea nchini
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Viongozi na wanachama wao waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa na kiusalama sasa warudi nyumbani baada ya Serikali kuwa imetoa tangazo bungeni.
"Tumepokea kauli ya Serikali iliyotolewa Bungeni juu ya hakikisho la usalama kwa viongozi na wanachama ambao walikimbia nje nchi kwa sababu za kiusalama na kisiasa. Sisi kama chama tunatoa mwito kwa wanachama na viongozi wetu kurejea nchini." alisema Mhe. John Mnyika
Mnyika amesema suala la viongozi hao wakimbizi lilikuwa moja ya ajenda ya Maridhiano.
Mnyika amewataja Tundu Lissu, Lema na Wenje kuwa ni miongoni mwa walio nje ya nchi na Chama kitawaandikia rasmi kuwapa utaratibu wa kurejea nyumbani.
No comments
Post a Comment