Afikishwa Mahakamani kwa kujifanya polisi na kumpiga polisi wa kweli
Mwanaume ambaye alijifanya kuwa afisa wa polisi kutoka makao makuu ya polisi Kenya amefikishwa mahakamani kwa makosa ya kumpiga na kumjeruhi afisa halisi wa polisi.
Pia alikabiliwa na mashtaka ya kujifanya kuwa afisa wa polisi.
Mtuhumiwa anadaiwa kujifanya afisa wa polisi ili kumuingiza kibaridi Obura.
Upande wa mashtaka ulisema kuwa mtuhumiwa ambaye alionekana kuwa mgeni alimwita konstebo Obura na kumwambia alikuwa afisa wa polisi kutoka makao makuu ya polisi.
Alipoambiwa
kujitambulisha kwa kutoa kitambulisho chake cha kazi, aliingiwa na uhayawani na
kumshambulia.
Afisa huyo wa polisi aliokolewa na wenzake ambao walimkamata Nyaanga na kumzuilia katika kituo cha polisi cha Lang’ata.
Alikanusha mashtaka hayo
mbele ya Hakimu Mkuu wa Kibera Ann Mwangi japo kupitia kwa waikili wake Mwihaki
Ng’ang’a, Nyaanga aliomba mahakama kumhurumia.
Wakili Ng’ang’a alisema
kuwa mtuhumiwa hana rekodi ya makosa na kwamba ni baba wa familia na mwananchi
mtiifu.
Ng’ang’a alisema kuwa
mtuhumiwa atazingatia masharti yote ya dhamana, mahakama hiyo ikimwachilia kwa
dhamana ya shilingi 30,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa
tena Juni 28.
No comments
Post a Comment