Atiwa mbaroni kwa kuua mpenzi wake gesti
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam
linamshikilia mwanaume mmoja aitwaye Heri Julius Kisaka wa miaka 33 ambaye ni
fundi simu na mkazi wa Mburahati kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke msusi.
Kamanda wa Jeshi la polisi Kanda maalum ya
Dar es salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo kwamba
mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua mwanamke aitwaye Leonia Julius Zerota
anayekadiriwa kuwa na miaka 30-33 msusi maeneo ya Sinza, Kinondoni.
Amesema tukio hilo lilitokea Juni 17, 2022
katika moja ya chumba kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Lavi Park iliyopo
Tegeta kwa Ndevu ambapo mwili wa marehemu ulikutwa ndani ya chumba hicho.
Kamanda amesema mtuhumiwa baada ya kutekeleza
mauaji hayo alifanikiwa kutoroka na ufuatiliaji ulipoanza alikamatwa akiwa
maeneo ya Manzese Jijini Dar es salaam.
Hata hivyo kamanda Jumanne Muliro amesema
chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa.
No comments
Post a Comment