Serikali imewahakikishia wanaohama Ngorongoro kuendelea na shughuli zao
Serikali
kupitia kwa Waziri
mkuu mhe.Kassim Majaliwa amewahakikishia wakazi wanaohama kwa hiari yao kutoka
katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kijiji cha Msomera, Handeni
Mkoani Tanga, kuendelea na shughuli zao za ufugaji katika mazingira yaliyo
bora.
Majaliwa
ameyasema hayo hii leo Juni 23, 2022 wakati akiwaaga wakazi wa Ngorongoro
wanaohama kwa hiari yao kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo hilo, katika
viwanja vya Ofisi Kuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA), Ngorongoro
Mkoani Arusha.
“Ninawaomba
msafiri kwa amani kabisa na mioyo yenu ikunjuke isikilizeni Serikali yenu
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan sasa hivi mko huru, nendeni mkakae
kwenye nchi yenu kwa uhuru,” amesisitiza.
Kwa
upande wake Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro, Dkt. Christopher Timbuka amesema awamu
ya pili ya zoezi la kuwahamisha wakazi wa eneo la Ngorongoro kwa hiari lilianza
Juni 20, 2022, ikihusisha jumla ya kaya 27 zenye watu 127 na mifugo 488
.
Amesema
hadi sasa kaya zilizohama kwa hiari katika eneo la Ngorongoro katika awamu ya
kwanza na ya pili ni 48 zenye jumla ya watu 233 na mifugo 899 na kwamba
utaratibu wa kuwahamisha umefanyika kwa kufuata hatua mbalimbali ikiwemo
kuhakiki idadi ya watu.
“Hatua
nyingine ni kusainisha vitabu vya fidia vya wakazi wanaohama kwa hiari awamu ya
pili, kuhakiki idadi ya mifugo na kuiweka alama ili iweze kusafirishwa pamoja
na kuhakiki na kutambua aina za nyumba za wakazi hao kwa ajili ya taratibu za
ubomoaji,” amefafanua Dkt. Timbuka.
Hata
hivyo, amesema mbali na kupewa nyumba, fidia na shamba, kaya zote zitapewa
magunia mawili ya mahindi kwa kwa kipindi cha miezi mitatu ili waweze kujikimu
kwa kipindi cha mpito wakati wakijiandaa na msimu wa kilimo.
Mmoja
wa wakazi wanaohama kwa hiari kutoka Ngorongoro kwenda Msomera, Emmanuel
Saitoti wa Kijiji cha Nainokanona, ameishukuru Serikali kwa upendeleo ilioutoa
kwao kwa kuwa mbali ya kupewa nyumba pia Msomera wanakwenda kupata fursa
zitakazowakuza kiuchumi.
Amesema,
“Serikali tunaishukuru imetupendelea sana, tumepata hati za nyumba na mashamba
pamoja fidia ya fedha, naishauri iendelee kuwahamasisha na wakazi wengine nao
wahame kule hakuna maendeleo. Msomera tunakwenda kufanya shughuli nyingi za
maendeleo.”
No comments
Post a Comment