"Tumeona baadhi ya maeneo kumekuwa na
changamoto, kwanza watu walipohesabiwa mwaka 2012 ,wengine hawakuhesabiwa ,sasa
Serikali inapopeleka fedha kama inalenga hospitali ,ujenzi wa shule, kuboresha
huduma inapeleka kwa idadi ya namba ambayo imeandikishwa ,kumbe idadi ya watu
ni kubwa ,sisi Umoja wa Vijana wajibu wetu mkubwa ni kuhakikisha tunaungana na
Serikali na kuwaleza Watanzania wote wakiwemo vijana wenzetu kwamba sensa ni
kitu muhimu na tunaisadia Serikali katika kusukuma ajenda ya maendeleo".
Amesema Bw.Kihongosi.
Amesisitiza vijana wajitokeze kwa wingi
lakini waende kuhamasisha wenzao kwasababu siku ya leo wamekuwa na vijana ambao
wanatoa elimu juu ya sensa,ambapo wanawakufunzi wa sensa kutoka serikalini
lakini wapo watu ambao wametunga nyimbo zinazohamasisha sensa na kueleza
umuhimu wa sensa .
"Kwa hilo ni jambo la pili na jambo la
tatu kampeni hii itakuwa endelevu hapa Dar es Salaam na kampeni tumezindua leo
tarehe 23 mwezi wa Sita lakini tutakwenda katika mikoa yote ya Kanda ya ziwa,
tutakwenda Kanda ya kaskazini , tutakwenda Kusini,lengo ni kuwakumbusha
Watanzania na wajue sensa ina umuhimu mkubwa katika maendeleo lakini pia
tutafika mpaka Zanzibar na kama ambavyo unafahamu Taifa letu ni Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania tumeungana Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kwa hiyo
tunawajibu kufika mpaka Zanzibar kwenda kuhamasisha vijana na Watanzania
kuhusiana na suala Zima la sensa.". Amessisitiza Bw.Kihongosi.
Aidha amesema katika elimu ya sensa kama kuna
Wizara ambayo inahusika na masuala ya kuratibu sensa ndio maana wameleta
watalaam kutoka serikalini ambao watagusa maeneo yote yanayohitajika kuhusu
sensa ,waeleza kwanini kuna sensa na inahesabiwa kwa Watanzania na kwanini pia
Wananchi wahesabiwe maana Watanzania wataenda kufahamu kumbe wakihesabiwa.
No comments
Post a Comment