Header Ads

Header ADS

Dkt Lwoga amshukuru rais samia kwa kuipatia makumbusho mwenyekiti wa bodi.



Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt Noel Lwoga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuteua Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo muhimu kwa uhifadhi na uelimishaji juu ya urithi wa asili na utamaduni wa nchi.

Dkt Lwoga pia Amempongeza Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Taasisi hiyo Dkt. Oswald Masebo kwa kuaminiwa na Mhe. Rais kwa nafasi hiyo muhimu kwa maendeleo endelevu ya Makumbusho ya Taifa na kuahidi kumtampatia ushirikiano wowote unahitajika.

Aidha, Dkt. Lwoga amewapongeza wafanyakazi wa Taasisi hiyo kwa kufanya kazi kwa moyo na kwa mafanikio makubwa yaliyopo na kuwataka kuongeza juhudi ya kazi ili kupata zaidi matokeo chanya kwa kuwa changamoto zilizotokana na kutokuwa na Mwenyekiti wa Bodi kwa zaidi ya miaka mitatu, sasa zimepata ufumbuzi.

“Kwa kupata bodi, sasa tumepata nguvu mpya, na hatutokuwa peke yetu kwenye safari ya kupelekea mabadiliko na matokeo stahiki kwa Taasisi yetu, hivyo kila mtumishi atafakari mabadiliko na mafanikio aliyoleta kupitia kazi yake katika kituo/Idara/Kitengo kwa Miaka mitatu iliyopita, na kuweka mikakati mipya kwa Mwaka 2022/2023 katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Taasisi wa Miaka Mitano, sasa kwa kasi mpya chini ya Bodi yetu. Kazi iendelee.” Alisema Dkt Lwoga

 


No comments

Powered by Blogger.