TPLB: Kanuni zitaamua mfungaji bora
Bodi
ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ imetoa ufafanuzi wa tuzo ya Mfungaji Bora kwa
msimu wa 2021/22, ambao utafikia tamati leo Jumatano (Juni 29) katika viwanja
vinane tofauti.
Hadi
sasa Mshambuliaji wa Mabingwa Young Africans Fiston Kalala Mayele na George
Mpole wanaendelea kupambana kuwania tuzo hiyo, huku kila mmoja akifunga mabao
16.
Afisa
Habari wa TPLB Karim Boimanda, amesema endapo wawili hao watamaliza msimu
wakiwa na mabao sawa ya kufunga, wataangalia kanuni ambazo zinatoa ufafanuzi
nani anapaswa kuwa mfungaji bora.
Boimanda
amesema: Ikitokea Fiston Mayele na George Mpole watamaliza msimu na magoli kama
yalivyo sasa (16), kikanuni Mayele ndiye atakuwa mfungaji bora kwa kuwa hana
goli la penati wakati Mpole ana penati mbili.”
Young
Africans itamaliza msimu wa Ligi Kuu 2021/22 kwa kucheza didi ya Mtibwa Sugar
Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku Mshambuliaji Fiston Mayele
akitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo iliyotwaa Ubingwa wa Tanzana
Bara.
Geita
Gold FC nayo itamaliza msimu kwa kucheza dhidi ya Coastal Union katika Uwanja
wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, huku George Mpole akitarajiwa kuwa sehemu ya
kikosi cha Kocha Fred Felix Minziro.
No comments
Post a Comment