Header Ads

Header ADS

Maiti kadhaa bado kupatikana baada ya ajali ya treni

 Miili ya watu wasiopungua watatu ilikuwa bado haijapatikana kufikia leo asubuhi, kufuatia ajali mbaya ya treni katika jimbo la Bavaria kusini mwa Ujerumani. 

Polisi imesema baadhi ya watu bado wanakosekana na kwamba idadi ya wale ambao hawajatolewa maelezo ni chini ya kumi. 

Msemaji wa polisi amesema walitarajia winchi yenye uwezo wa kubeba hadi tani 120 kuwasili kwenye eneo la ajali hiyo, na kusema hawaondowi uwezekano wa kuwa na wahanga zaidi chini ya mabehewa yalioharibiwa vibaya, ambapo juhudi za mara mbili kuyainua zimeshindikana.

Ijumaa mchana mabehewa kadhaa ya treni inayofanya safari zake kati ya mikoa yaliacha njia katika kijiji cha Burgrain wakati treni hiyo ikielekea mjini Munich na kusababisha vifo vya watu wanne kati ya 40 waliokuwemo ndani ya treni hiyo, huku 40 wakijeruhiwa, wakiwemo watoto kadhaa.--




No comments

Powered by Blogger.