Header Ads

Header ADS

Waziri Prof .Mbarawa kuwa mgeni rasmi kongamano la wakandarasi wazawa

 Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Chama Cha  Wakandarasi Wazawa  (ACCT) litakalofanyika Juni 4, 2022 jijini Dodoma lenye lengo la kumpongeza Rais Samia kwa kutwaa tuzo ya ujenzi wa miondombinu na kuifanya Tanzania kutambulika Kimataifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini  Leo Juni 3 jijini Dodoma Mwenyekiti wa ACCT Thobias Kyando amesema kongamano lililoandaliwa na wakandarasi wazawa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia.

"Rais Samia alistahili kabisa kupewa tuzo hii ya heshima kwasababu amefanya mambo makubwa katika sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara, na bandari ndio maana akaibuka kidedea wa tuzo hiyo na sisi tukiwa wadau wa miundombinu tunampongeza sana,"amesema

Amesema  ujenzi wa miundombinu imekuwa na faida hasa kwa wandarasi Wazawa kwasababu wanahusika moja kwa moja kuiboresha pindi wakandarasi wageni wanapoondoka.

Mwenyekiti huyo ameiomba  Serikali kuendelea kuwaamini wakandarasi wazawa kwa kuwapatia tenda mbalimbali ili waendelee kupata uzoefu hiyo itasaidia kuipunguzia serikali gharama ambazo imekuwa ikitumia kutoa tenda kwa kampuni za nje ya nchi.

"Ni vyema wakandarasi wazawa wakawa wanahusika moja kwa moja katika kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchi  hiyo  itasaidia serikali kutumia fedha kidogo na kupata uzoefu kutoka kwa wakandarasi wa kigeni,"amesema.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa ACCT  Profesa Mhandisi John Bula  alisema wamendaa kongamano kubwa litakalofanyika katika ukumbi wa Jakaya kikwete Dodoma lengo ni kutoa pongezi kwa Rais Samia kwa kutwaa tuzo ya heshima.

Kesho ni pongezi kubwa kwa Rais wetu kwa kupata  tuzo kubwa ambayo inatupa nguvu kwasababu hata sisi wakandarasi wazawa ameendelea kutujali kwa kutupatia kazi mbimbali za ujenzi  tunachoomba tupewe fursa zaidi ili tuonyeshe uwezo zaidi kwasababu utaalamu unaweza ukanunuliwa kutoka nje kwa pale tutakapokwama,"alisema

Naye Mwanachama wa ACCT Maida Waziri amesema tuzo aliyoipata Rais Samia ni tuzo kubwa watanzania hawanq budi kuendelea kutambua na kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika sekta ya miundombinu.

Amesema kupitia tuzo hiyo Dunia imeweza kumtambua hivyo kama watanzania lazima kutambua umuhimu wa kile alichopewa Rais Samia na kutembe kifua mbele kwasababu haikuwa kazi rahisi kuchukua tuzo hiyo.

"Tuzo hiyo ameipata kutokana na ujenzi wa miundombinu kwa kweli tuna haki ya kujivunia sana kwa sababu kama watanzania Rais Samia ameleta tuzo hiyo kubwa napenda kusema kuwa watanzania  tunaona dira na muelekeo wa serikali ya awamu ya sita tunaona njia kubwa huko tunakoenda,"amesema

Maida amesema kigezo cha nchi kuonekana ni tajili mara nyingi hupimwa kwenye ujenzi wa miundombinu na kwa tuzo hiyo ambayo Rais Samia ameipata ameonyesha watanzania  kuwa Tanzania ni  nchi  tajiri.

"Rais Samia amepewa tuzo na Benki ya Afrika imetambua jitihada anazozifanya katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo miradi aliyoikuta iliyoanzishwa na  hayati Dk.John magufuli na kuanzisha miradi mipya,"ameeleza

 





No comments

Powered by Blogger.