Header Ads

Header ADS

Matukio ya Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto Makambako Mkoani Njombe yawaibua UWT

   Kutokana na kukithiri kwa matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya mji wa Makambako na maeneo mengine mkoani Njombe.
Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoani humo imeendelea kupaza sauti yao na kuviomba vyombo vya serikali kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya matukio ambayo yanaendelea kuongezeka huku pia wakiitaka jamii kuelimika na kuachana na vitendo hivyo.
Hayo yamebainishwa na wanawake wa jumuiya hiyo ya Chama cha Mapinduzi kwenye mkutano wa mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Bi,Skolastika Kevela na baadhi ya wajumbe,viongozi na madiwani katika halmashauri ya mji wa Makambako uliofanyika katika ofisi za Chama tawi la Ubena mjini humo.
Lucy Mbogela na Magreth Mfilinge ni miongoni mwa wajumbe waliotoa kilio chao dhidi ya matukio hayo huku wakibainisha kuwa katika halmashauri hiyo tatizo hilo limekuwa ni kubwa na kubainisha kuwa ndani ya miezi mitatu pekee kumeripotiwa kesi 57 za unyanyasaji.
“Kuna tatizo kubwa la unyanyasaji wa wanawake na watoto,ukienda kituo cha polisi pale ni foleni ya kesi za unyanyasaji na wanawake wale wanakosa msaada wa kisheria mpaka unakuta unyanyasaji hauishi”walisema wanawake
Aidha katibu wa jumuiya hiyo mkoa wa Njombe Bi,Rehema Mbwana ametoa wito kwa maafisa ustawi wa jamii kushirikiana zaidi na jamii pamoja na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia ili kuongeza mapambano dhidi ya ukatili.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Njombe Bi,Scolastika Kevela ameonyesha kusikitishwa na kulia pamoja na wanawake hao huku akiomba jamii kubadirika na kuwataka wanawake kuongeza kasi ya kujitafutia uchumi binafsi kwa kuwa matukio mengi ya ukatili huo yamekuwa yakijitokeza kwa wanawake na watoto wao kutokana na utegemezi.
“Hii inasikitisha sana lakini niwaase kina mama tumiliki uchumi,tukimiliki uchumi baadhi ya matukio kwenye maeneo yetu yatapungua lakini Njombe ni matajiri wa Parachichi,mtu ukiwa na ekari moja huangaiki hata kidogo,niwasisitize tuhakikishe tunapata angalau ekari moja ya parachichi”alisema Bi,Kevela.
Mwenyekiti huyo ameendelea na ziara yake katika halmashauri ya Makambako mara baada ya ziara hiyo kuifanya katika halmashauri ya Wanging’ombe na Ludewa huku ikiwa lengo lake ni kukutana na kuzungumza na viongozi wa jumuiya hiyo katika halmashauri zote za mkoa wa Njombe



No comments

Powered by Blogger.