Mbaroni kwa kujifanya mkuu wa mkoa wa Mbeya
Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya linamshikilia Warren Max Mwinuka (20) Mkazi wa Makondeko,Mbeya Mjini kwa
tuhuma za kujifanya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera akitumia
akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la “juma_homera”.
Mtuhumiwa alikamatwa
mnamo tarehe 07.06.2022 majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Mama John
Jijini Mbeya.
Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwaadaa watu kwa kujifanya ni Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu yake ili wananchi waweze kutoa/kupeleka kero/shida mbalimbali kwake.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara
baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.
Imetolewa na,
Kamanda wa Polisi
SACP – Ulrich Matei
MKOA WA MBEYA.
No comments
Post a Comment