Mtanzania kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema
Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila
Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi.

Dk Mwigulu amebainisha hayo bungeni jijini Dodoma,
wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na
matumizi kwa mwaka 2022/23.
Waziri huyo amesema ili kufikia azma hiyo wataanza kutoa
namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania kuanzia umri
wa kuanzia miaka 18 kwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa
(NIDA) unaomtaka kila mwananchi mwenye umri huo wa au zaidi kujisajili.
“Napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa
(wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye
miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya
nchi,”amesema
Waziri huyo amefafanua kuwa kila mwenye namba ya mlipakodi
atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya
mtandao.
No comments
Post a Comment